Sunday, October 17, 2010

MHE.HAWA NG'HUMBI AITINGISHA MBEZI,MSUGURI

Mgeni rasmi Mhe.Shamsa Mangunga akmnadi Bi Hawa Ng'humbi mgombea Ubunge wa Jimbo la Ubungo kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika uwanja wa Mkutano Viwanja vya Mbezi kwa Msuguri, hii niishara ya kuonyesha Wana CCM wake kwa waume wanapendana.
Mhe.Hawa Ng'humbi akielezea ilani ya chama Cha Mapinduzi na kuwaomba ridhaa Wananchi wakichague Chama Cha Mapinduzi kwa kuwa ndio chama kilichosimama imara, akiwataka Wananchi wachague mafiga matatu, ikiwa Ngazi ya Uraisi Mhe.Dr Jakaya Mrisho Kikwete, Ngazi ya Ubunge yeye Mwenyewe Bi.Hawa Ng'humbi kwa Jimbo la Ubungo na Mwisho aliomba wachaguliwe Madiwani wote wakata  zote za CCM.
Baada ya mgeni rasmi kuingia meza kuu wote waki simama kuonyesha ishara ya heshima.kwa mgeni rasmi huku wakimshangilia kwa makofi na vigerere wengine wakisema "USHINDI NILAZIMA 2010" hawalali mpaka kieleweke...!

No comments:

Post a Comment